2014-05-12 11:56:13

Jipyaisheni katika upendo unaobubujika kutoka katika Damu Azizi ya Yesu!


Yesu Kristo alionesha upendo mkuu kwa binadamu kwa kuyamimina maisha yake kwa njia ya mateso, kifo na ufufuko, ili kumkirimia mwanadamu maisha ya uzima wa milele.

Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii anasema kwamba, waamini wamekombolewa kutoka katika lindi la dhambi na mauti kwa njia ya Damu Azizi ya Yesu Kristo. Anawaalika waamini kujipyaisha katika upendo unaobubujika kutoka katika Damu Azizi ya Yesu.







All the contents on this site are copyrighted ©.