Kiongozi wa UNDP aliyeko ziarani nchini Tanzania, Helen Clark, amesema usimamizi wa
maliasili unaoshirikisha jamii ni ufumbuzi wa muda mrefu na wenye ufanisi zaidi kwa
ya kudhibiti vitendo vya ujangili wa tembo na biashara haramu ya wanyamapori. Akizungumza
Jumapili tarehe 11 Mei 2014 na watu kutoka vijiji 21 karibu na Hifadhi ya Taifa Ruaha
alijifunza uzoefu wao na changamoto za usimamizi katika uhifadhi wa wanyamapori.
'Ni wazi,' alisema, 'kila mtu katika jamii, ikiwa ni pamoja na wanawake, vijana na
wazee, wana wajibu katika uendelezaji wa ulinzi wa wanyamapori na jamii karibu na
maeneo ya hifadhi. Mipango ya jamii lazima ipewe msaada inayostahili ili kuzalisha
mapato kwa ajili ya watu wa vijijini na kusaidia kuleta njia mbalimbali za mapato
kupitia utalii na sekta nyingine za huduma, 'alisema.
Helen Clark alitembelea
Hifadhi ya Taifa Ruaha, Iringa, mkoa uliopo kusini mwa Tanzania kuangalia matokeo
ya mradi wa uhifadhi wa UNDP na Mfuko wa Dunia wa Mazingira uliolenga uhifadhi wa
wanyamapori na mazingira ya Kusini mwa mzunguko wa Tanzania, ikiwa ni pamoja na maeneo
ya hifadhi ya Ruaha, Kitulo, Mpanga Kipengere na Mlima Rungwe.
Kupitia msaada
wa UNDP wa kiufundi na fedha, mradi ulifanya sensa ambayo ilionesha kupungua kwa dhahiri
kwa idadi ya tembo katika mfumo wa ikolojia wa Ruaha-Rungwa, ikiwa ni upungufu kutoka
tembo 31,625 mwaka 2009 hadi 20,090 tu mwaka 2013. Kwa hiyo mradi ulianzisha shughuli
za kuisaidia Wizara ya Maliasili na Utalii katika maendeleo ya mkakati wa taifa wa
kupambana na biashara ya wanyamapori.
Msaada wa UNDP uliwezesha ununuzi wa
matingatinga. Uongozi wa Hifadhi umeanza uboreshaji wa barabara ambao utafungua eneo
hilo kwa ajili ya kuongeza fursa za utalii, usalama bora zaidi, na vilevile kuwezesha
doria ya mara kwa mara kwa ajili ya kupambana na ujangili.
Sehemu kubwa ya
kazi hii imekuwa kuimarisha utawala katika taasisi za kitaifa zinazohusika na usimamizi
wa wanyamapori na utekelezaji; kuimarisha maisha ya jamii na mipango ya kugawana faida
ili kupunguza kichocheo kwa jamii hizo kuajiriwa katika shughuli za ujangili unaofanywa
na magenge ya wahalifu.