2014-05-11 09:32:36

Papa anawaombea wasichana waliotekwa nyara Nigeria


Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii anapenda kuungana na wananchi wa Nigeria pamoja na Jumuiya ya Kimataifa kusali kwa ajili ya kuachiliwa kwa wasichana mia mbili waliotekwa nyara na Kikundi cha Boko Haram nchini Nigeria hivi karibuni.

Hii ni kampeni ya kimataifa ambayo inawahusisha viongozi mbali mbali na watu maarufu, ili kushinikiza Kikundi cha Boko Haram kuwaachilia huru wasichana waliotekwa, ili waweze kujiunga na familia zao na hatimaye kuendelea na masomo yao!







All the contents on this site are copyrighted ©.