Ufaransa kula sahani moja na vikundi vya kigaidi Afrika!
Waziri wa ulinzi wa Ufaransa Jean Ives Le Drain anasema kwamba, Ufaransa itapeleke
kikosi cha wanajeshi elfu tatu, Kaskazini mwa Afrika ili kupambana barabara na vikundi
vya kigaidi ambavyo vimeendelea kusababisha maafa makubwa kwa wananchi wa Afrika
ya Kaskazini.
Kikosi cha askari elfu moja, kitaendelea kubaki nchini Mali,
ili kuhakikisha ulinzi na usalama wa wananchi na mali zao. Itakumbukwa kwamba, wanajeshi
kutoka Ufaransa wako nchini Mali tangu Januari 2013 baada ya Umoja wa Mataifa kuomba
Ufaransa kusaidia juhudi za kudumisha amani nchini Mali na katika nchi jirani.