Bwana Alfonso Dhlakama Mwenyekiti wa Chama cha Upinzani cha RENAMO nchini Msumbiji
ni kati ya viongozi waliojiandikisha katika kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu unaotarajiwa
kufanyika Mwezi Oktoba, 2014 nchini Msumbiji. Kwa kutangaza nia ya kushiriki katika
uchaguzi mkuu, Bwana Alfonso Dhlakama ametoka rasmi mafichoni ambako alikuwa amejificha
baada ya hali ya kisiasa nchini Msumbiji kuanza kuchafuka tena kwa RENAMO kutishia
kurudi tena msituni ili kuendesha vita.
RENAMO imetangaza kusitisha mashambulizi
katikati ya Msumbiji, ambako kwa miaka miwili, RENAMO kimekuwa kikipambana na Jeshi
la Serikali ya Msumbiji. Eneo linalohusika kadiri ya taarifa ya vyombo vya habari
ni katika Jimbo la Sofala, Msumbiji.