2014-05-08 10:54:43

Mshikamano wa kidugu na wananchi wa Syria


Baraza la Kipapa la Familia kwa kushirikiana na Shirika la Misaada la Kanisa Katoliki Italia, Caritas linaendelea kuhamasisha upatikanaji wa amani kwa ajili ya familia za wananchi wa Syria, kwa kuwataka wahusika wakuu kujikita katika majadiliano ili kumaliza vita hii ambayo imeendelea kusababisha maafa makubwa kwa wananchi wasiokuwa na hatia.

Wanataka pia watu wote waliotekwa nyara kuachiliwa huru. Caritas Italia itaendelea kutoa msaada wake wa hali na mali kwa wanachi wa Syria katika kipindi hiki kigumu pamoja na kusaidia jitihada za kuwafunda watu umuhimu wa amani na mshikamano wa dhati.

Baraza la Kipapa la Familia pamoja na Caritas, Italia linatoa ujumbe huu ambao uko kwenye mfumo wa video kwenye Maonesho ya Vitabu yanayofanyika kuanzia tarehe 8 hadi tarehe 12 Mei, 2014 huko mjini Torino, Kaskazini mwa Italia. Vatican inashiriki pia katika maonesho ya vitabu huko Torino kama mjumbe wa heshima.







All the contents on this site are copyrighted ©.