2014-05-08 11:07:53

Marehemu Askofu mkuu Franklin azikwa mjini Luanda!


Askofu mkuu Damiao Antonio Franklin wa Jimbo kuu la Luanda, Angola aliyefariki dunia tarehe 28 Aprili 2014 nchini Afrika ya Kusini, ambako alikuwa anapata matibabu, amezikwa kwa heshima zote za Kanisa, Jumatatu, tarehe 5 Mei 2014 mjini Luanda. Ibada ya Misa Takatifu imehudhuriwa na Maaskofu Katoliki Angola, waamini na viongozi wa Serikali wakiongozwa na Rais Josè Eduardo Dos Santos wa Angola.

Marehemu Askofu mkuu Franklin alizaliwa tarehe 6 Agosti 1950 huko Cabinda. Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi, akapadrishwa kunako mwaka 1978. Akateuliwa na Papa Yohane Paulo II kuwa Askofu msaidizi wa Jimbo kuu la Luanda, Angola kunako mwaka 1992.

Mtakatifu Yohane Paul II akamteuwa kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Luanda, Angola kunako mwaka 2001. Ameshiriki kikamilifu katika maadhimisho ya Awamu ya Pili ya Sinodi ya Maaskofu wa Afrika iliyofanyika mjini Vatican kunako Mwaka 2009.







All the contents on this site are copyrighted ©.