Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican anatarajiwa tarehe 8 Mei 2014 kuongoza
Ibada ya Rozari Takatifu, muhtasari wa Injili kwa maelfu ya waamini na watu wenye
mapenzi mema watakaokuwa wamekusanyika kwenye Madhabahu ya Bikira Maria wa Pompei,
Napoli, Kusini mwa Italia. Waamini watasali sala iliyotungwa na na Mwenyeheri Bartolo
Longo kunako mwaka 1883.
Waamini kuanzia tarehe 6 Mei 2014 wameanza maadhimisho
ya Jubilee ya Miaka 75 tangu kutabarukiwa kwa Kanisa kuu la Pompei kwa maadhimisho
ya Ibada ya Misa Takatifu, mkesha na sala ya Rozari Takatifu. Kardinali Pietro Parolin
anatarajiwa kuongoza Ibada ya Misa Takatifu Alhamisi, tarehe 8 Mei 2014 na baadaye
sala ya Rozari takatifu majira ya mchana.
Ibada hii inatarajiwa kuhudhuriwa
na Maaskofu kutoka Kusini mwa Italia, waamini pamoja na viongozi mbali mbali wa Serikali