Tume ya Makardinali inayodhibiti Benki ya Vatican, IOR, Jumatatu tarehe 28 Aprili
2014 amefanya kikao chake cha kawaida, ili kuweka mbinu mkakati wa utekelezaji wa
shughuli zake katika Benki hii. Tume hii imeamua kwamba, itakuwa inakutana mara tatu
kwa mwaka, kama hakutakuwa na jambo la dharura litakaloilazimisha tume hii kukutana
nje ya utaratibu huu.