Padre Federico Lombardi, Msemaji mkuu wa Vatican anasema maandalizi ya maadhimisho
ya kutangazwa kwa Wenyeheri Yohane XXIII na Yohane Paulo II kuwa watakatifu yataanza
kutimua vumbi siku ya Jumamosi, mikesha itakayofanywa kwenye Makanisa mbali mbali
mjini Roma, kielelezo cha mshikamano wa maisha ya kiroho. Ibada katika Makanisa zitaendeshwa
katika lugha mbali mbali.
Ibada ya Misa takatifu inatarajiwa kuhudhuriwa na
Viongozi na wawakilishi wa dini na madhehebu mbali mbali ya Kikristo, kuna wajumbe
93 wanaowakilisha nchi 24 na kati yao kuna viongozi wakuu wa Serikali, Malikia na
Wafalme. Makardinali 150, Maaskofu 1000. Kuna Mapadre 870 watakaoshiriki kugawa Ekaristi
Takatifu
Jumapili asubuhi, Ibada itaanza kwa Rozari ya Huruma ya Mungu, hapo
saa 3:00 asubuhi, ikisindikizwa na nyimbo kutoka katika kwaya mbali mbali za Roma,
Bergamo na Poland.