2014-04-24 16:19:23

Waziri mkuu wa Albania Bwana Edi Rama akutana na kuzungumza na Papa Francisko mjini Vatican


Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi tarehe 24 Aprili 2014 amekutana na kuzungumza na Waziri mkuu wa Albania Bwana Edi Rama, ambaye baadaye amekutana pia na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican aliyekuwa ameambatana na Askofu mkuu Dominique Mamberti, Katibu mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican.

Viongozi hawa wawili wamezungumzia kuhusu uhusiano kati ya pande hizi mbili, lakini zaidi wakajikita katika tema zinazogusia masuala ya kimataifa, kikanisa na kiraia: Wameangalia kwa pamoja umuhimu wa majadiliano ya kidini na mchango wa Kanisa katika ustawi na mafao ya wengi nchini Albania. Wamegusia pia masuala ya kikanda na safari inayotekelezwa na Albania ili kuweza kujiunga na Umoja wa Ulaya.







All the contents on this site are copyrighted ©.