2014-04-21 10:57:09

Yohane XXIII na Yohane Paulo II ni moto wa kuotea mbali!


Meya wa Jiji la Roma Ignazio Marino anasema, Jiji la Roma limekwishajiandaa kwa ajili yakuwapokea wageni na mahujaji watakaoshiriki katika Ibada ya Misa Takatifu kwa ajili ya kuwatangaza Weenyeheri Yohane XXIII na Yohane Paulo II kuwa watakatifu hapo tarehe 27 Aprili 2014. Mabus zaidi ya 2000 yanatarajiwa kuingia mjini Roma, lakini hadi sasa kuna Mabus 500 tu ndiyo yaliyokwisha sajiliwa. Mabus ambayo hayakusajiliwa hayataruhusiwa kuingia mjini kati!

Waziri wa mambo ya ndani wa Italia anasema kwamba, Ibada hii inatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi wakuu wa Serikali 19, Mawaziri wakuu 24 na wajumbe 61 wanaowakilisha nchi 54 kutoka sehemu mbali mbali za dunia. Umati wa watu uliokuwa umefurika katika maadhimisho ya Siku kuu ya Pasaka kwa Mwaka 2014 mjini Vatican, kilikuwa ni kipimo cha Jiji la Roma kujipanga vyema kwa ajili ya kukabiliana na umati mkubwa wa watu watakaofika mjini Roma kwa ajili ya Ibada ya Misa Takatifu ya kuwatangaza Wenyeheri Yohane XXIII na Yohane Paulo II kuwa Watakatifu.







All the contents on this site are copyrighted ©.