Ujumbe wa Papa wa Pasaka wawakumbuka wanaoteseka kwa njaa, vita na uonevu.
Baba Mtakatifu Francisko, katika Jumapili ya kwanza ya Pasaka, ya Huruma Takatifu,
mapema aliongoza Ibada ya Misa, katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro. Ibada
ilihudhuriwa na umati wa watu zaidi ya 150,000. Baada ya Ibada hiyo majira ya adhuhuri
kama kawaida ya siku hii kwa Mapapa, kutokea dirisha lake la kujisomea, alitoa ujumbe
na baraka zake za Pasaka kwa Jiji la Roma na Dunia kwa Ujumla, Urbi et Orbi .. Katika
ujumbe huo amesema, Ndugu zangu wapendwa, Heri ya Siku Kuu Takatifu ya Pasaka! Kanisa
duniani kote, limetafakari maneno ya Malaika kwa wanawake. Msiogope, Nafahamu mnamtafuta
Yesu aliyesulubiwa. Hayuko hapa. Maana amefufuka. Njoni, muone mahali alipokuwa amelazwa
"(Mt 28:5-6 ). Msiwe na woga wala hofu! Bwana Mfufuka !
Papa amefafanua kwamba,
hiki ndicho kilele cha tangazo la Injili, Ni habari Njema, : Yesu, ambaye alisulubiwa,
amefufuka ! Tukio hili ni msingi wa imani ya Mkristo na tumaini lake. Kama Kristo
asinge fufuka , Ukristo ulikuwa umepoteza maana yake ; ujumbe na utume wote wa kanisa
ungekuwa ni bure , kwa kuwa, Ufufuko wa Kristo, ndiyo jambo msingi la kwanza katika
Utume wote ya Kanisa tangu mwanzo wake kuendelea milele yote, kwamba Kristo amekishinda
kifo na kutuletea uzima wa milele. Huo ndiyo ujumbe, Wakristo wanaoutoa kwa dunia
leo hii: Yesu , Upendo wa Mungu uliomwilishwa, na aliye sulubiwa Msalabani , kwa
ajili ya dhambi zetu, lakini Mungu Baba Yake na Bwana wa maisha na kifo, alimfufua.
Kwa jina la Yesu , Upendo ameshinda juu ya chuki, huruma juu ya dhambi, wema juu ya
maovu , ukweli juu ya uwongo, maisha juu ya kifo.
Na hiyo ndiyo maana Wakristo
huwaambia watu wote, “Njoo nyote na muone, watu wa kila hali ya maisha ya binadamu
,wanaojiweza, wadhaifu na wanyonge, wenye dhambi na mlio walio katika hali ya kifo
, Habari Njema ni kwenu nyote! NI maneno ya ushahidi wa ushindi mwaminifu wa upendo,
unaotutaka kuondoka katika maisha ya kale na kukutana na watu wengine, kuwa karibu
na wale wanao angamizwa kwa matatizo ya maisha , kushirikiana na masikini , wale walio
simama kando ya upande wa wagonjwa, wazee n.k " Njoo! uone Upendo wenye nguvu zaidi
, Upendo wenye kutoa uzima wa milele, upendo wa matumaini ya maua katika jangwa.
Kwa
hakika hii furaha katika mioyo yetu, na leo hii pia wewe tunakuambia, Bwana kufufuka.
Baba Mtakatifu baada ya maelezo hayo , alitoa wito kwa watu wote, waliwezeshe Kanisa
kuwafikia na kuwapa habari kwamba kuna Baba wala si yatima, kwamba Kanisa linawapenda
kuwaalika kuabudu pamoja nawe.
Papa pia ametoa wito kwa wahusika wote , watoe
msaada wa kushinda janga la njaa , hasa linachochewa na uwepo wa migogoro na matumizi
mabaya ambayo mara nyingi ni binadamu kukosa kuwajibika. Kuliwezesha Kanisa kulinda
mazingira magumu , hasa watoto, wanawake na wazee, kama matokeo ya dhuluma unyanyasaji
na kutelekezwa. Pia kuliwezesha Kanisa kutoa huduma kwa ndugu na dada zetu waliopigwa
na mlipuko wa ugonjwa Ebola katika Guinea Conakry, Sierra Leone na Liberia, na pia
kutoa huduma kwa wanaosumbuliwa magonjwa mengine mengi ambayo pia huenezwa kwa sababu
ya kutelekezwa na umaskini.
Pia Papa ameomba Faraja kwa wale ambao hawawezi
kusherehekea hii Pasaka na wapendwa wao kwa sababu ya ukosefu wa haki , haki yao
imechanwa, na upendo wao kunyakuliwa , kama ilivyo kwa watu wengi , wakiwa ni makuhani
na waamini, walio sehemu mbalimbali za dunia, ambao wametekwa nyara, na wakimbizi
pia, watu waliolazimika kuhama makazi yao ya kudumu na sasa wanaishi katika hali duni
za kusikitisha, ubinadamu wao ukifinyangwa finyagwa na kukosa hata uhuru wa kukiri
imani yao kwa uhuru.
Tunakuomba , Bwana Yesu, ukomeshe vita, kila migogoro,
iwe mikubwa au ndogo, ya kale au ya hivi karibuni.
Na kwa namna ya pekee papa
aliitaja taifa pendwa la Syria linalopita katika wote mateso na madhara ya mgogoro
wa kisiasa, ili watu wa eneo hilo wasiokuwa na hatia waweze kupokea msaada wa kibinadamu
na kwamba, kusitisha utumiaji wa nguvu mauti , hasa dhidi ya watu wasio weza kujitetea
wenyewe , badala yake wajawe na ujasiri wa kujadili amani ya muda mrefu, muafaka
wa muda mrefu unao subiriwa. Papa pia aliitaja migawanyiko na vurugu katika taifa
la Iraki, Israel na Palestina.
Pia aliligeukia bara ya la Afrika na kuomba
kwa ajili ya kufikishwa mwisho migogoro katika Jamhuri ya Afrika ya Kati na mashambulizi
ya kikatili ya kigaidi katika maeneo ya Nigeria na vitendo vya unyanyasaji katika
Sudan ya Kusini.
Na pia uwepo wa nyoyo za maridhiano na kindugu katika taifa
la Venezuela.
Kwa ufufuko Bwana , ambamo mwaka huu Wakristu wa makanisa yote
wamesherehekea Siku Kuu hii pamoja na wale wanao fuata kalenda ya Juliana, Bwana
na aangazie nakuvuvia juhudi za kukuza amani Ukraina ili kwamba wale wote wanaohusika
katika jumuiya ya kimataifa waweze kufanikisha juhudi za kuzuiia ghasia , katika
roho ya umoja na mazungumzo, na kuonesha njia kwa ajili ya baadaye ya nchi , kama
ndugu na kwamba wote waweze kupaza sauti zao na kusema, Christos Voskrese !" [ Kristo
Kafufuka !]