Turudi Galilaya kuigundua upya Neema ya Mungu- Papa
Baba Mtakatifu Francisko, amehimiza waamini kutafakari upya maana ya wito wao katika
ubatizo , alikokuita “kurudi Galilaya”, kuyasoma upya maisha ya Yesu katika misingi
ya msalaba na ushindi wake, kwa tendo kuu la upendo. Papa alieleza katika homilia
yake, wakati akiongoza Maadhimisho ya Mkesha wa Pasaka katika Kanisa Kuu la Mtakatifu
Petro, mjini Vatican . Ametoa wito kwa kila Mkristu kugundua upya neema za ubatizo
wao kama chemichemi ya maisha , yanayochota nguvu kutoka vyanzo vya imani na uzoefu
wa maisha ya Kikristo. Kurudi Galilaya inamaanisha ni kurudi zaidi ya yote katika
mwanga ule ambamo mna neema ya Mungu iliyougusa moyo tangu mwanzo wa kujiunga katika
hija ya maisha ya Kikristo. Papa alieleza kuwa, Injili ya ufufuo wa Yesu Kristo
huanza na safari ya wanawake kaburini alfajiri siku baada ya Sabato. Wao walikwenda
kaburini, kwa ajili ya kutoa heshima zao kwa mwili wa Bwana , lakini waliona kaburi
li wazi na tupu . Malaika mmoja mwenye nguvu akawaambia : "Msiongope ninyi, kwa maana
najua kuwa mnamtafuta Yesu aliyesulubiwa. Hayupo kwani amefufuka kama alivyosema.....
(Mt 28:5) nendeni mkawaambie wanafunzi wake, amewatangulia Galilaya " (V. 7) .
Wanawake haraka waliondoka na njiani walikutana na Yesu aliyewaambia msiogope ; nendeni
mkawaambie ndugu zangu waende Galilaya ; wao huko wataniona "(mstari 10).
Baada
ya kifo cha Mwalimu wao, wanafunzi wa Yesu walitawanyika ; imani yao alikuwa imeshuka,
kila jambo lilioonekana kama kufikia ukomo wake, walikosa uhakika na matumaini yao
kuwa kama yamekufa. Lakini sasa, ujumbe wa wanawake wa kushangaza kama ilivyokuwa,
uliwafikia kama mwali wa mwanga mkali katika giza nene. Habari ya Yesu kufufuka ilienea
kama alivyosema. Na hata ile habari ya kwenda Galilaya waliyokuwa wameisikia wanawake
mara mbili, kwanza kutoka kwa malaika na kisha kutoka kwa Yesu mwenyewe: Waende Galilaya
;huko watamwona, inawachoma moyo. .
Papa alikumbusha Galilaya palikuwa ni
mahali wanafunzi walipoitwa kwa mara ya kwanza. Na sasa ni kurudi huko, mahali ambako
waliitwa mara ya kwanza, ambako Yesu akitembea katika mwambao wa ziwa , aliwaona wavuvi
wakitwika nyavu zao , na kuwaita na waliacha nyavu zao , wakamfuata (cf. Mt 4:18-22)
.
Papa anafafanua kwamba , kurudi Galilaya maana ya kutafakari upya yote, kwa
misingi ya msalaba na ushindi wake . Tena ni kusoma kila kitu - mahubiri ya Yesu ,
miujiza yake, jamii mpya , msisimko na usaliti huu, hata usaliti mpya, ni kusoma
kila kitu kuanzia mwanzo hadi mwisho , matendo yote ya upendo wa Yesu, hadi tendo
hili kuu la upendo .
Pia kwa kila mmoja wetu, kuna Galilaya ya asili katika
njia ya kumfuata Yesu. Nendeni Galilaya ina maana ya jambo njema , likiwa na maana
ya kugundua upya maana ya ubatizo wetu kama chemichemi ya maisha, ni kujenga nguvu
mpya, kutoka vyanzo vya imani yetu na maisha yetu ya Kikristo . Kurudi Galilaya maana
yake ni wote kurudi katika kuuona mwanga mkali wa neema ya Mungu, iliyonigusa mwanzo
na kujiunga katika mwanzo wa safari ya wokovu. . Kutoka nguvu hiyo , nikaweza kuwasha
moto wa imani unaomlika leo na kila siku , na kuleta joto na mwanga kwa ndugu zangu
wake kwa waume. Kutoka mwali wa moto huo , mmezaliwa furaha wanyenyekevu, furaha isiyoweza
kufadhaishwa na huzuni au dhiki, ila ni furaha nzuri , furaha ya upole.
Katika
maisha ya kila Mkristo , baada ya ubatizo kuna pia Galilaya moja nzuri zaidi ya wa
kukutana binafsi na Yesu Kristo ambaye aliyeniita kua mfuasi wake na kushiriki katika
utume wake. Kwa maana hii, kurudi Galilaya inakuwa ni kumbukumbu ninayotakiwa kuiweka
kama hazina ya thamani sana ndani ya kina cha moyo wangu , Yesu alipopita katika njia
yangu, na kunitazama kwa huruma akaniomba kumfuata. Ina maana kufufua kumbukumbu
ya wakati huo Wakati macho yake alikutana, wakati alipofanya mie nijisikie na kutambua
kwamba ananipenda.
Papa alimalizia homilia yake akisema, , Usiku wa leo ,katika
usiku huu, kila mmoja wetu anaweza kujiuliza , Je, ni ipi Galilaya yangu? Je, wakumbuka
au umesahau? Je, limekwenda katika njia zilizonifanya kusahau Galilaya ?Basi na tumwombe
Bwana , atupe msaada wa kukumbuka Galilaya yetu, kwa utambuzi kwamba, tunataka kurudi
huko, kukutana na mwenyewe, aliyetuvutia kwa huruma yake.
Injili ya Pasaka
ni wazi kabisa: tunahitaji kwenda huko , kumwona Yesu aliye fufuka , na kuwa mashahidi
wa ufufuo wake. Hii si kurudi nyuma katika muda ; si aina ya kuchosha. Lakini ni kurudisha
upendo wake kwetu kwa ajili ya kuupokea moto wa Yesu unaomulikia dunia na kuuleta
mwanga huo kwa watu wote na hadi miisho yote ya dunia . Galilaya ya mataifa (Mt
4:15; Isaya 8:23) ! Upeo wa Bwana Mfufuka, upeo wa Kanisa; hamu kali ya kukutana
naye. Shime tushike mwendo wa kwenda Galilaya! Katika Ibada hii, Papa alibatiza
Wakatukumeni kumi, kati yao akiwemo mtoto wa miaka saba raia wa Italia na mtu mzima
mwenye umri wa miaka 58 kutoka Vietnam. Wabatizwa wengine ni raia wa Ufaransa, Belarus,
Lebanon na Senegal.