2014-04-20 07:56:03

Mchakato wa majadiliano kati ya Serikali na RENAMO yanatia moyo!


Chama cha upinzani cha RENAMO nchini Msumbiji kinaendelea kufanya majadiliano na serikali, ili kiweze kushirikishwa katika vikosi vya ulinzi na usalama katika ngazi zote. Haya ni kati ya maamuzi yaliyofikiwa hivi karibuni kati ya Serikali ya Msumbiji na Chama cha RENAMO, maamuzi ambayo yataanza kutekelezwa kwa usaidizi wa Jumuiya ya Kimataifa.

Serikali ya Msumbiji inasema kwamba, uamuzi uliofikiwa na RENAMO ni hatua kubwa katika mchakato wa majadiliano kati ya Serikali na RENAMO iliyokuwa inatishia kurudi tena msituni, hali ambayo ingechafua msingi wa maendeleo uliokuwa umefikiwa tangu kusitishwa kwa vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini Msumbiji kunako mwaka 1992.







All the contents on this site are copyrighted ©.