Wasichana 114 bado wanashikiliwa na Kikundi cha Kigaidi cha Boko Haram
Habari zilizokuwa zimetolewa na Jeshi la Nigeria kwamba, watoto wa shule waliokuwa
wametekwa nyara hivi karibuni kutoka shule ya Chibok wameachiliwa huru si za kweli
na kwamba, wasichana hao bado wanashikiliwa na Kikundi cha Kigaidi cha Boko Haram,
ambacho bado kinaendelea kusababisha majanga makubwa kwa wananchi na mali zao.
Taarifa
zinaonesha kwamba, kati ya watoto 115 kati ya wasichana 129 waliokuwa wametekwa hawajulikani
mahali alipo. Hayo yamesemwa na Asabe Kwanbura, Mwalimu mkuu wa shule ya wasichana
ya Chibok. Ni wasichana 14 tu waliopatikana hadi wakati huu tunapoandika taarifa hii
baada ya kuwatoroka watekaji wao na kutokomea msituni. Wasichana wengine 115 bila
shaka bado wako mikononi mwa wateka nyara wao.