2014-04-19 15:04:58

Salini kwa ajili ya watu waliozama na kufa maji nchini Korea


Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii, anawaalika kuungana naye katika sala, ili kuwaombea watoto waliokufa maji nchini Korea ya Kusini pamoja na familia zao hapo tarehe 19 Aprili 2014. Hivi karibuni, Meli iliyokuwa imebeba abiria 475, kati yao wanafunzi 325 waliokuwa kwenye safari ya masomo, walizama maji.

Hadi sasa maiti 29 zimekwishapatikana na wengine 268 bado hawajulikani waliko, lakini inahofiwa kwamba, watakuwa wamekufa maji! Hadi sasa kuna jumla ya watu zaidi ya 550 wanahusika katika zoezi la kuwatafuta watu waliozama baharini. Chanzo cha ajali hii bado hakijajulikana, lakini serikali inaendelea bado kufanya uchunguzi.







All the contents on this site are copyrighted ©.