2014-04-19 08:17:38

Kesha la Pasaka, 2014 mjini Vatican


Baba Mtakatifu Francisko anatarajiwa kuongza Ibada ya mkesha wa Pasaka kuanzia saa 2:30 Usiku kwa saa za Ulaya. Atabariki moto na baadaye kuingia kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, huku akiwa amebeba Mshumaa wa Pasaka, kielelezo cha Yesu Mfufuka. Itaimbwa Mbiu ya Pasaka kutangaza ukuu wa Mshumaa wa Pasaka, "Exsultet" na baadaye Liturujia ya Neno la Mungu itafuata.

Monsinyo Guido Marini, Mshehereshaji wa Ibada za Kipapa anasema kwamba, itafuatia Liturujia ya Ubatizo. Baba Mtakatifu Francisko anatarajiwa kubatiza Wakatekumeni wapya kumi kutoka Jimbo kuu la Roma. Kati yao, Wakatekumeni 5 ni kutoka Italia, wengine ni wale wanaotoka Bielrussia, Senegal, Lebanon, Ufaransa na Vietnam. Baada ya hapo itafuatia Liturujia ya Ekaristi Takatifu. Baba Mtakatifu ataadhimisha Ibada hii akisaidiana na Makardinali, Maaskofu na Mapadre.

Taarifa zinaonesha kwamba, Baba Mtakatifu Francisko katika Sherehe za Pasaka ya Bwana anatarajiwa kuongoza Ibada ya Misa Takatifu kuanzia majira ya saa 10: 15 asubuhi kwa saa za Ulaya na baadaye atatoa ujumbe wake kwa mji wa Roma na ulimwengu, maarufu kama "Urbi et Orbi". Maadhimisho ya Pasaka kwa Mwaka 2014 yana vionjo ya Kiekumene.







All the contents on this site are copyrighted ©.