Baba Mtakatifu atoa zawadi ya Mayai ya Pasaka wa watoto waliolazwa Hospitali ya "Bambino
Gesu"
Ijumaa Lori lililojaa mayai maalum ya kipindi cha Pasaka ambayo ndani yake yamejazwa
chokoleti, moja kwa moja kutoka Vatican , lilipakua mzigo wake katika Hospitali ya
Rufaa ya Watoto ya Bambino Gesù . Mayai hayo ni zawadi ya Papa Francisko kwa watoto
waliolazwa katika hospitali hiyo, walau waweze kutoa tabasamu la kufurahia Siku Kuu
ya Pasaka. Shehena hiyo ya mayai makubwa yapatayo 150 ilitolewa kwa watoto waliolazwa
katika idara ya Saratani. Zawadi hii ni ishara ya mawazo mapya ya Papa Francisko
kwa watoto wagonjwa katika hospitali hiyo ambayo aliitembelea wakati wa Mkesha wa
Noeli mwaka jana 2013, Desemba 21. Baba Mtakatifu bado anaona hai moyoni mwake, tabasamu
na kicheko cha watu siku hiyo alipopandisha katika hospitali hiyo iliyoko katika kilima
cha Gianicolo, hapa Roma , ambako alizungukwa na kundi la waamini, Wauguzi na madaktari
, wanaojihusika na utoaji wa huduma kwa watoto wadogo wagonjwa waliolazwa katika
hospitali hiyo. Hospitali hii ya jijini Roma, ni mali ya Jimbo la Papa tangu mwaka
1924, na inajulikana kama Hospitali ya Papa . Na Hospitali hiyo kwa mara ya kwanza
iliwekwa katika uangalizi wa Papa Yohana XXIII, Na hivyo kuwa urithi wa Mapapa wote
waliofuatia. Na Papa Francisko, Noeli iliyopita alirudisha utamaduni wa kutembelea
watoto waliolazwa katika hospitali hiyo , inayojulikana kama Hospitali ya Papa.