2014-04-18 15:24:01

Amani ni dharura halisi kwa Mashariki ya Kati na Dunia.


Amani ni dharura ya kwanza kwa Mashariki na kwa dunia nzima leo hii. Ni hoja inayokuwa na uzito wa kipekee hasa kwa jumuiya ya Wakristo, hata katika miaka ya hivi karibuni zaidi , kama ilivyoshuhudiwa na Syria. Ni wito kwa Dunia, uliotolewa na Kardinali Leonardo Sandri , Mkuu wa Usharika kwa ajili ya Makanisa ya Mashariki. Wito huu ameutoa wakati akihojiwa na gazeti la Vatican, juu ya historia ya makutano ya amani kati ya Mungu na binadamu, na baina ya mtu na mtu na tofauti zao zote, zilizokwisha onekana katika historia ya binadamu.
Kardinali Leonardo Sadri pia ameeleza amani ni moja ya kipengele kinachoongoza ziara ya Papa Francisko atakapo tembelea Mashariki ya Kati. Kardinali, anaelezea pia umuhimu wa makusanyo ya sadaka ya Ijumaa Kuu kwa ajili ya Nchi Takatifu.
Amesema, makusanyo ya sadaka kwa ajili ya kusaidia maeneo takatifu ni moja ya utendaji muhimu zaidi ya kwa kanisa la Yerusalemu na katika Nchi Takatifu, kwa maana ya kuufanikisha uongozi wa makanisa kutoa huduma kiroho na kimwili. Na hivyo inakuwa na maana ya kushirikishana na kugawana kilichopo kwa ajili ya utendaji mzuri wa kanisa kiroho na kihali pia. Na katika mtazamo wa kina kwa Nchi Takatifu, badala ya fedha, hasa ni wakati wa kushirikiana katika sala na urithi wa kumbukumbu katika msaada wa utume wa kawaida wa pamoja . Kutoka katika hili Wakristo wanaoishi katika Nchi Takatifu, wanapata mwangwi wa kwanza wa kuitangaza Injili kwa bidii zaidi, wakiwa wameshikamana na ndugu zao, wake kwa waume, katika imani na katika kuwa walinzi, wakiwa wameshikana katika umoja na wachungaji wao . Na hivyo Baba Mtakatifu Francisko, wakati akiupokea Ujumbe wa Usharika mwezi Novemba, alisema kuwa kila Mkatoliki ana deni la shukrani kwa Makanisa yanayodumu kuwepo katika Mkoa wa Mashariki ya Kati. Wakristu wana deni la kuyaheshimu kwa sababu ndani mwake wanaouona mwanzo wao.

Na kwa nini Sadaka ya Ijumaa Kuu? Kwa kuwa Siku hii ni siku ya ukimya wa Yesu. Ni siku inayotoa kumbukumbu kali ya zawadi yake kuu ya sadaka ya maisha. Siku ambayo alitangaza kwamba yote yamekamilika. Na kama yote yamekalishwa , kinachobaki kuzungumzia ni upendo tu katika ukamilifu wake. Ni kama upendo ulioonekana wakati wa kimya katika Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, Jumapili ya matawi ya mwaka huu, wakati wa liturujia ya Neno iliyotangaza mateso ya Yesu na kifo chake msalabani.

Kardinali Sadri wakati huo alikumbuka mateso ya Yesu n na pia mawazo yake yalikwenda kwa wanaoteseka kwa wakati huu, kama ilivyokuwa kwa Padre Frans van der Lugt , Mjesuit Mholanzi, alieuawa siku chache zilizopita huko Homs Syria. Na ndivyo ilivyo kwa watu wengi, waliouawa au kuaathirika bila hatia katika Nchi Takatifu . Damu isiyokuwa na hatia inaendelea kunyunyiza kwa ajili ya kutangaza amani itokayo kwa Mungu. Na pia uchungu wa moyo ulikwenda kwa Kiongozi wa Kanisa la Kiotodosi la Syro- Askofu Youhanna Ibrahim , na pia kwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiotodosi al Kigrikii , Boulos Yazigi , waliotekwa nyara pamoja na Mapadre wawili , Maher Mahfuz,Kanisa la Kigiriki- . na Michel Kayyal wa Kanisa Katoliki la Armenian , mwanafunzi katika Kipapa Armenian College na wengine wengi wasiojulikana kwa majina. Kardinali Sadri amesema daima wanamwomba Bwana wa Amani awaangazie maana ya matukio haya, ili mateso yao yasiwe ya bure.

Na wana tumaini na kukutana upya kati ya Papa Francisko na Patriaki Bartholomayo I, mwezi Mei, kwamba uakuwa ni wakati mzuri wa kuzama zaidi katika sala , kama wafanyakazi wasiochoka kuombea amani duniani. Na kwamba wanaliweka tumaini hili katika maombezi ya Wenye Heri Yohana XXIII na Yohana Paul II, ambao hivi karibuni watatajwa Watakatifu. Amani , bado ni dharura na kipaumbele cha kwanza kwa Mashariki ya Kati na kwa dunia.








All the contents on this site are copyrighted ©.