2014-04-17 08:29:27

Ijumaa kuu ni Siku ya Mapumziko Cuba


Serikali ya Cuba imeridhia kwamba, Ijumaa kuu, Siku ambayo Wakristo sehemu mbali mbali za dunia wanakumbuka: mateso na kifo cha Yesu Kristo Msalabani, iwe ni Siku kuu ya Kitaifa na kwamba, wananchi wa Cuba watapumzika. Uamuzi huu wa Serikali ulipitishwa kwenye kikao cha Bunge, kilichofanyika mwezi Desemba, 2013.

Sheria hii itaanza kutumika rasmi mwezi Juni, 2014, lakini kama ilivyotokea kunako Mwaka 2012 na Mwaka 2013 wananchi wa Cuba katika Siku kuu ya Ijumaa kuu kwa Mwaka huu watapumzika pia.







All the contents on this site are copyrighted ©.