Katekesi ya Papa - hili ni Juma la kutembea katika njia ya Yesu ya Msalaba
Baba Mtakatifu Francisko ametoa Katekesi yake kwa mahujaji na wageni ,kama ilivyo
kawaida ya Jumatano. Papa aliangalisha mafundisho yake katika matukio ya Juma hili
Takatifu, akisema Liturujia inaturejesha katika matukio ya huzuni na kusikitisha
kama ilivyokuwa katika somo la Injili , Yuda anakwenda katika baraza la viongozi na
kumsaliti bwana wake, kwa kudai kulipwa fedha kuifanya kazi ya kuonyesha mahali alipo
bwana wake .
Papa Francisko anasema, kitendo hicho cha Yuda, maisha ya Yesu
yanakuwa na thamani kubwa. Ni tendo la kuhuzunisha lililo kuwa ishara ya mwanzo wa
mateso ya Kristo , njia ya chungu, ambayo yeye aliichagua kwa hiari na uhuru wake
wote. Yeye mwenyewwe alisema waziwazi , nitayatoa maisha yangu kwa ajili yenu
... na hakuna mtu aliye lazimisha, licha ya kuwa na uwezo kuyatoa na uwezo wa kuyarudisha
tena "(Yn 10:17-18).
Na hivyo ndivyo alivyo anza kutembea katika njia kudhalilishwa
na kusalitiwa. Yesu aliyatoa maisha yake kama bidhaa ya sokoni kwa bei ya dinari
30. Na Yesu katika njia hii ya aibu na fedheha kuliko njia zote. Yesu alitembea juu
ya njia ya udhalilishaji na madhulumu, yaliyofikisha kilele cha maisha yake hapa duniani.
Baba Mtakatifu Fransciko aliendelea kuzungumzia njia hii ngumu aliyopita
Yesu, akisema kilele cha udhalilishaji huo, wa mauti ya msalaba, mauti mabaya zaidi
yaliyokuwa yanadhamiriwa kwa ajili ya watumwa na wahalifu, yanamfika Yesu aliye hesabiwa
kama nabii , anakufa kama mhalifu.
Papa anasema, kwa kumtazama Yesu katika
mateso yake, inakuwa ni kioo cha kuyaona pia yetu na mateso ya watu wote, na pia
kupata jibu la Mungu kwa siri ya uovu, maumivu, na kifo. Na mara nyingi tunafikiri
juu ya vitisho vya majaribu na maumivu katika mazingira yetu na kuuliza, " Kwa
nini Mungu karuhusu ? Mateso ya Yesu yanakuwa ni jeraha la kina kwa ajili yetu ,
kwa ajili ya kutafakari maana ya mateso na kifo , hasa kwa wale wasiokuwa na wasio
na hatia !
Papa ameeleza na kutaja, ni mara ngapi tunaona au kusikia habari
za watoto wanaoteseka, na watu waliojeruhiwa mioyoni. Ni siri ya uovu, na Yesu anachukua
mabaya haya yote, mateso yote yawe juu yake. Wiki hii, sisi itakuwa vizuri kwa kila
mmoja wetu kwa kuangalia msalaba, kumbusu majeraha ya Yesu, akambusu msalaba. Alichukua
juu yake yote ya mateso ya binadamu, kuwa mateso ina huvaliwa.
Tunatarajia
kwamba Mungu katika nguvu zake ushindi wa haki dhidi uovu na mateso , ni ushindi wa
milele usiokoma wala kuwa na kipimo. Mungu anaonyesha ushindi wa unyenyekevu kwamba,
huushindia ubinadmau wote. . Mwana wa Mungu , kwa kweli, inaonekana juu ya msalaba
kama kushindwa mtu mateso, ni kusalitiwa , kutukanwa, na hatimaye kufa. Lakini Yesu
aliruhusu hili ili aweze kuyachukua mabaya yote mwenyewe na juu yake mwenyewe kutoa
jibu la ushindi. Mateso yake ni si ajali; kifo chake si kifo cha kawaida , lakini
ilikuwa imeandikwa hivyo . Hii ni siri ya Mungu , siri ya kushangaza ya unyenyekevu
wa Mungu. Kwa maana Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwana wake wa pekee "
( Yohana 3:16 ).
Kwa maelezo hayo, Baba Mtakatifu ametoa mwaliko kwa waamini
wote , tunapoendelea na maadhimisho ya Juma Takatifu, kumfuata Yesu katika njia
hii ya msalaba na kuiga unyenyekevu wake wenye upendo mkuu katika kutimiza mapenzi
ya Baba yake, na hasa wakati wa magumu na mateso , na kuifungua mioyo yetu kwa zawadi
ya sakramenti ya toba na upatanisho na ukombozi na maisha mapya. Yeye alifanya hivyo
kwa ajili yangu. " NI kubusu msalaba na kusema : "Kwangu mimi . Asante Yesu kwa ajili
yangu".Ni kuchukua msalaba katika mkono yetu, kuumbusu mara nyingi na kusema " Asante
Yesu , asante Bwana, na "iwe hivyo".