2014-04-16 16:09:29

Kardinali Pietro Parolin, aongoza Ibada ya Misa kuwakumbuka wafia dini wapya


Jumanne 15 Februari 2014, majira ya Jioni, Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican, aliongoza Ibada ya Misa kwa nia ya kuwakumbuka Mashahidi wote wapya wafia Dini, waliotolea maisha yao kwa ajili ya Injili popote duniani, katika miaka ya hivi karibuni . Tukio hili liliandaliwa na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio katika Kanisa la Mtakatifu Bikira Maria la Trastevere Roma .
Kwa mwaka huu pia, kina cha moyo wa maadhimisho ya Juma Takatifu kwa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio , ni kuwakumbuka mashahidi wa Ukristo wengi, walio tawanyika katika maeneo mengi mbalimbali ya dunia ambako wanakabiliwa na mateso , ubaguzi, kunyimwa uhuru wa dini na hata ya maisha. Pia jumuiya inafanya kumbukumbu kwa walio athirika na rejea, kwa kuzingatia maneno ya Papa Francis aliposema: ". Leo, hii katika karne ya ishirini na moja , Kanisa letu limekuwa Kanisa la mashahidi, kama ilivyo onyesha katika miezi ya hivi karibuni huko , Pakistan, Indonesia, Nigeria, Kenya , Tanzania, Afrika ya Kati”
Katika homilia yake, Kardinali Parolini amesema, ni katika mataifa haya na mengine mengi, ambako Wakristo wasiokuwa na silaha, watu watulivu na wasiopenda kufanya vurugu wamekuwa kafara, kwa sababu ya imani yao ya Kikristu. Wakristo hao wanapambanishwa na dhuluma, ghasia, rushwa na ugaidi. Watu waliouawa kwa sababu ya kwenda kusali kanisani, au katika mashule ya Kikristo yaliyo chomwa moto,na ambako wanaishi kwa kvitisho vya kufungwa magerezani, au kuuawa, kwa sababu majitoleo yao ya kuelimisha vijana na makundi ya uhalifu kwamba Yesu Kristu ni Bwana wa Amani.
Hawa ni Mashahidi wa imani ya karne wa Karne ya ishirini na moja, wanaume na wanawake ambao wanatuonyesha sisi nguvu ya upinzani dhidi ya maovu hadi kutoa zawadi ya maisha ; Wakristo ambao mara kwa mara, wametoa ushuhuda wa kitume, " Hatuwezi kuacha kuyanena mambo tuliyoyaona na kusikia."

Ibada hii iliyoandaliwa na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio , ilihudhuriwa na wawakilishi wa Makanisa na jamii ya Kikristo wa madhehebu yote na kuongozwa na Kardinali Pietro Parolin , Katibu wa Jimbo la Papa.









All the contents on this site are copyrighted ©.