2014-04-15 07:39:39

Wasi wasi wazuka Nigeria kuhusu matumizi ya silaha za kemikali


Jumuiya ya Kimataifa inaitaka Serikali ya Nigeria kufanya upembuzi yakinifu kuhusiana na madai kwamba, katika mapambano Kaskazini mwa Nigeria imegundulika kwamba, kumekuwepo pia na matumizi ya silaha za kemikali, kama ilivyoelezwa na Bwana Gabriel Suswam, Gavana wa Jimbo la Benue, Nigeria wakati alipokuwa anatoa taarifa yake kwa Tume ya ulinzi na usalama ya Seneti ya Nigeria hivi karibuni.

Matumizi ya silaha za kemikali yasipodhibitiwa mapema anasema Gavana Suswam hakuna nchi jirani inayoweza kuwa na uhakika wa usalama wa maisha ya raia wake. Nigeria inapaswa kuwahakikishia wananchi wa Nigeria na Jumuiya ya Kimataifa kwamba, silaha za Kemikali zilizotumika si kwa ajili ya maangamizi ya halaiki ya watu pamoja na kufahamu madhara yanayoweza kusababishwa na matumizi ya silaha hizi kwa maisha ya watu.

Nigeria imetoa ombi maalum kwa Umoja wa Mataifa kusaidia kufanya uchunguzi wa kina kuhusiana na madai ya matumizi ya silaha za kemikali, Kaskazini mwa Nigeria.








All the contents on this site are copyrighted ©.