Zaidi ya watu sabini na mmoja wamepoteza maisha na wengine mia moja na ishirini na
wanne kujeruhiwa vibaya kutokana na mlipuko wa bomu uliotokea kwenye kituo kikuu cha
Mabas, mjini Abuja, Nigeria, siku ya jumatatu, tarehe 14 Aprili 2014. Idadi ya watu
waliofariki dunia inatarajiwa kuongezeka maradufu. Huu ni mwendelezo wa mashambulizi
ya kigaidi yanayoitikisa Nigeria, licha ya mikakati ya Serikali kupambana na vitendo
vya kigaidi vinavyoendeshwa na Kikundi cha Boko Haram nchini Nigeria.
Takwimu
zinaonesha kwamba, tangu mwezi Januari hadi sasa kuna zaidi ya watu elfu moja na mia
tano ambao wamekwisha poteza maisha kutokana na mashambulizi ya vitendo vya kigaidi,
wengi wao ni raia wasiokuwa na hatia.