2014-04-13 11:19:41

Monsinyo Guido Marini kuendelea kuwa mshereheshaji wa Ibada za Kipapa


Baba Mtakatifu Francisko ameridhia uteuzi wa Monsinyo Guido Marini kuendelea kuwa ni mshereheshaji wa Liturujia za Kipapa. Itakumbukwa kwamba, Monsinyo Marini aliteuliwa na Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto wa kumi na sita, tarehe 1 Oktoba 2007 na amekuwa akishiriki katika maandalizi na maadhimisho ya Liturujia na Ibada mbali mbali zinazoadhimishwa na Baba Mtakatifu ndani na nje ya Vatican.

Monsinyo Guido Marini alizaliwa kunako tarehe 31 Januari 1965 huko Genoa, Kaskazini mwa Italia.







All the contents on this site are copyrighted ©.