Professa Margaret Scotford Archer, ateuliwa kuwa ni Rais Baraza la Kipapa la Taasisi
za sayansi Jamii
Baba Mtakatifu Francisko amemteua Professa Margaret Scotford Archer, kuwa Rais wa
Baraza la Kipapa la Taasisi za Sayansi Jamii. Professa Archer alizaliwa tarehe 20
Januari 1943. Baada ya masomo yake kwa miaka mingi alikuwa ni Jaalimu wa Sayansi Jamii
nchini Uswiss. Kunako tarehe 19 Januari 1994 akateuliwa na Mwenyeheri Yohane Paulo
II kuwa mjumbe na muasisi wa tume hii.
Professa Archer ni mtafiti katika nyanja
za Falsafa Jamii pamoja na Nadharia za Kijamii. Ni mwandishi mashuhuri wa vitabu na
majarida mbali mbali duniani.