2014-04-11 14:18:21

Kipimo cha ukimwi kuanza kuuzwa dukani.. Uingereza..


Uingereza imepitisha sheria inayo idhinisha maduka ya dawa , kuuza vifaa vya kipimo cha HIV, ili mtu kujipima mwenyewe nyumbani, kuona iwapo ana virusi vya HIV au hapana. Hatua hii ni kwa ajili ya kusaidia watu kukabiliana na virusi vya HIV. Hata hivyo vifaa hivyo bado havijapatikana madukani.

Taarifa inasema, kupitishwa kwa sheria hii, maana yake imerahisisha zaidi watu kutambua hali zao katika maradhi ya ukimwi, wenyewe nyumbani. Hapo awali, iliruhusiwa watu kupata majibu yao kwa huduma ya online nyumbani.
Ni matumaini ya Serikali y aUingereza kwamba kwa kupishwa sheria ya mtu kujipima mwenyewe, kutalisaidia taifa kutambua idadi ya watu wanaoishi na VVU .
Kipimo hiki kinatajwa kuwa chepesi cha mtu kujichua tone la damu kutoka kidoleni na kuipima. Na majibu ya damu hiyo , yataonyesha iwapo ana virus au la.








All the contents on this site are copyrighted ©.