2014-04-10 14:55:19

Balozi Zvonimir Jankuloski awasilisha hati zake za utambulisho mjini Vatican


Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi tarehe 10 Aprili 2014 amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Balozi Zvonimir Jankuloski wa Jamhuri ya Watu wa Yugoslavia ya zamani mjini Roma. Balozi Jankuloski alizaliwa tarehe 7 Oktoba 1958, ameoa na mtoto mmoja. Kwa taaluma ni mwanasheria aliyehitimu masomo yake ya uzamivu kunako mwaka 1990.

Katika maisha yake amefanya kazi mbali mbali kama msaidizi wa Mahakama ya Wilaya mjini Skopje, Jaalimu wa somo la uhusiano wa kimataifa, mshauri katika masuala ya haki msingi za binadamu Barani Ulaya; mtafiti katika masuala ya wahamiaji; mkuu wa usalama wa taifa, Balozi na mwakilishi wa kudumu katika Baraza la Ulaya na ni mwandishi wa vitabu kadhaa.







All the contents on this site are copyrighted ©.