2014-04-08 12:02:22

Monsinyo Fabio Fabene ateuliwa kuwa Askofu


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Monsinyo Fabio Fabene, Katibu mkuu msaidizi wa Sekretarieti ya Sinodi za Maaskofu kuwa Askofu. Askofu mteule Fabio Fabene alizaliwa kunako tarehe 2 Machi 1959 mjini Roma. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 26 machi 1984 akapewa Daraja Takatifu la Upadre. Tangu wakati huo alipangiwa shughuli mbali mbali katika maisha na utume wa Kanisa.

Tarehe Mosi, Januari 1998 akaanza utume wake kwenye Baraza la Kipapa kwa ajili ya Maaskofu na Mwaka 2010 akaendelea kuwa ni Katibu mwambata Sekretarieti ya Baraza la Makardinali. Tarehe 8 Februari 2014, akateuliwa na Papa Francisko kuwa Katibu mkuu msaidizi wa Sinodi ya Maaskofu. Kitaaluma ni mwanasheria na mwandishi mzuri wa vitabu.







All the contents on this site are copyrighted ©.