2014-04-05 14:07:03

Papa asikitishwa na watawa watatu kutekwa nyara Kaskazini mwa Cameroon


Baba Mtakatifu Francisko amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kutekwa nyara kwa Mapadre wawili wa kutoka Jimbo Katoliki Vincenza, Kaskazini mwa Italia waliokuwa wanafanya utume wao nchini Cameroon, kama Mapadre wa Zawadi ya Roho Mtakatifu, "Fidei Donum" pamoja na mtawa mmoja kutoka Canada.

Baba Mtakatifu anaendelea kufuatilia habari hizi kwa kuwasiliana na Ubalozi wa Vatican nchini Cameroon. Watawa hawa watatu wametekwa nyara wakiwa kwenye makazi yao, Jimbo Katoliki la Maroua, Kaskazini mwa Cameroon na Kikundi cha watu kinachosaidikiwa kuwa na uhusiano na Kikosi cha Kigaidi cha Boko Haram.







All the contents on this site are copyrighted ©.