Maaskofu Katoliki Tanzania washiriki kwenye Njia ya Msalaba Kanisa kuu la Mtakatifu
Yohane wa Laterano, Roma
Baba Mtakatifu Francisko, Jumamosi tarehe 5 Aprili 2014 amekutana na kuzungumza na
Kundi la Pili la Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania linaloundwa na Jimbo kuu la
Songea. Itakumbukwa kwamba, Kanisa la Tanzania linaundwa na Majimbo makuu matano yaani:
Jimbo kuu la Dar es Salaam, Jimbo kuu la Tabora; majimbo yaliyoundwa kunako tarehe
23 Machi 1953. Askofu Marko Mihayo, akawa Askofu mkuu wa kwanza Tanzania kwa kupewa
Jimbo kuu la Tabora. Majimbo makuu kuu ya Mwanza na Songea yaliundwa kunako Mwaka
1978 na Mwaka 1999 Jimbo kuu Katoliki Arusha likaundwa.
Maaskofu Katoliki
kutoka Tanzania, Ijumaa jioni, wameshiriki kwenye Njia ya Msalaba kwenye Kanisa kuu
la Mtakatifu Yohane wa Laterano, lililoko mjini Roma, ambalo pia ni Makao makuu ya
Jimbo kuu la Roma.
Maaskofu wanasema, kwa kweli wanajisikia nyumbani kuzungumza
na Baba Mtakatifu Francisko, kwani mtindo wake wa majadiliano unajikita katika maisha
ya kijumuiya: kwa kuulizana, kushirikishana, kuhabarishana na kufafanuliana, ili kujenga
na kuliimarisha Kanisa la Kristo nchini Tanzania, ili liweze kuwa kweli ni chombo
cha kutangaza Injili ya Furaha. Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania linafanya hija
ya kitume mjini Vatican kuanzia tarehe 4 hadi tarehe 7 Aprili 2014 kadiri ya ratiba
elekezi. Maaskofu wafuatao wamekutana na kutetea na Baba Mtakatifu Francisko mjini
Vatican Jumamosi tarehe 5 Aprili 2014.
* Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa, Askofu
wa Jimbo Katoliki Iringa na Msimamizi wa Kitume, Jimbo kuu Songea.
* Askofu
Bruno Pius Ngonyani, Jimbo Katoliki la Lindi
* Askofu Evaristo Marc Chengula,
Jimbo Katoliki la Mbeya
* Askofu John Chrisostom Ndimbo, Jimbo Katoliki la
Mbinga aliyeambatana na Askofu mstaafu Emmanuel A. Mapunda
* Askofu Gabriel
Mmole, Jimbo Katoliki Mtwara
* Askofu Alfred Leonhard Maluma, Jimbo Katoliki
Njombe
* Askofu Castor Paul Msemwa, Jimbo Katoliki Tunduru-Masasi
*
Askofu Bernardin Mfumbusa, Jimbo Katoliki Kondoa
* Askofu Desiderius M. Rwoma,
Jimbo Katoliki Bukoba na Msimamizi wa Kitume Jimbo Katoliki Singida.