2014-04-04 07:29:56

Malikia Elizabeth II akutana na kuzungumza na Papa Francisko mjini Vatican


Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi jioni tarehe 3 Aprili 2014 amekutana na kuzungumza na Malkia Elizabeth wa pili wa Uingereza pamoja na ujumbe wake, waliopokelewa na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican baada ya kumaliza ziara ya kikazi kwenye Ikulu ya Italia. Mazungumzo kati ya Baba Mtakatifu na Malkia Elizabeth wa Pili anasema Padre Federico Lombardi, Msemaji mkuu wa Vatican kwamba, yamedumu kwa takribani dakika ishirini.

Viongozi hawa wawili wamebadilishana zawadi kama kielelezo cha kumbu kumbu yaziara ya Malikia Elizabeth wa Pili mjini Vatican. Baada ya mazungumzo na Baba Mtakatifu Malkia Elizabeth alirejea tena London, Uingereza. Hii ilikuwa ni ziara ya masaa machache lakini yenye umuhimu mkubwa katika kudumisha ushirikiano wa kimataifa.







All the contents on this site are copyrighted ©.