2014-04-03 10:45:04

Askofu mkuu Franco Coppola, Balozi Mpya wa Vatican Chad


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Franco Coppola kuwa Balozi Mpya wa Vatican nchini Chad na ataendelea kuwa pia ni Balozi wa Vatican nchini Jamhuri ya Watu wa Afrika ya Kati. Haya ni maeneo ambayo yamekumbwa na vita pamoja na kinzani za kijamii. Uteuzi huu unaonesha jinsi ambavyo Baba Mtakatifu Francisko anavyoguswa na mahangaiko ya watu wanaoteseka kutokana na majanga mbali mbali ya maisha.







All the contents on this site are copyrighted ©.