2014-04-02 12:35:11

Papa ahitimisha mzunguko wa Katekesi zake juu ya Sakramenti ya Ndoa.


Katika Katekesi yake ya Jumatano hii kwa mahujaji na wageni, Baba Mtakatifu alitangaza kukamilisha mzunguko wa mafundisho yake juu ya Sakramenti, na Sakramenti ya Ndoa. Alisema Sakramenti hii, inatuongoza katika kuona kiini cha mpango wa Mungu, ambao ni mpango wa agano na umoja na Mwenyezi Mungu.
Papa alieleza na kurejea yaliyoandikwa katika kitabu cha Mwanzo, ambamo mna maelezo jinsi Mungu alivyo anzisha familia ya mme na mke. “Mungu akaumba mtu kwa mfano wake , kwa mfano wa Mungu alimwumba : mwanaume na mwanamke aliwaumba” ... Na hivyo, mwanamume atamwacha baba yake na mama yake na kuambatana na mke wake , nao watakuwa mwili mmoja "( Mwa 1:27 ; 2:24). Papa ameeleza kwamba , kumbe binadamu ameumbwa kwa upendo kama kielelezo cha Mungu na upendo wake kwa binadamu . Na katika ndoa,ambao ni muungano wa mwanamume na mwanamke, kunatimizwa wito huu kama ishara ya usawa na ushirika wa maisha kamili hadi kilele chake.
Hata hivyo ni lazima kujiuliza , ndoa ina umuhimu gani kama sakramenti ? Na ndani ya maisha ya wanandoa mna nini ?
Papa ametoa majibu katika maswali hayo akisema, , kwanza , wakati mwanaume na mwanamke wanapoadhimisha sakramenti ya ndoa mbele ya Mungu na mbele ya Kanisa ,wanandoa hao wanatoa nje hisia zao za ndani, tendo hilo linakuwa ni kielelezo wazi cha upendo wao wa ndani, kama ilivyo kwa Mungu katika nafsi zake tatu, ushirika wa Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, anayeishi milele na milele katika umoja kamili.Na hii ndiyo siri ya ndoa: ni maisha ya nafsi tatu, Mungu, mme na mke, kama Biblia inavyosema, wanakuwa mwili mmoja" - kwa mfano wa upendo wake, kwa jina la Mungu katika ushirika unaochota kutoka asili yake na nguvu zake. .
Papa alieleza na kuhoji , iwapo wanandoa, bibi na bwana harusi ,wanalikumbuka hili? Na iwapo wanatambua zawadi hii kubwa ambayo Bwana amewapa. Zawadi halisi ya harusi. Papa aliwataka wana ndoa kutafakari maisha yao ya ndoa,kwa kuangalisha katika ushariki wa Utatu Mtakatifu, na kwa neema ya Kristo, Mungu aliye hai, aminifu na upendo wake .
Papa aliendelea kueleza kwamba, Mtakatifu Paulo, katika barua yake kwa Waefeso, anasisitiza ndoa imara kwa Mkristu, kama ulivyo uhusiano imara kati ya Kristo na Kanisa, (taz. Efe 5 0.21-33 ). Na hii ina maana kwamba ndoa, ni kuitikia wito maalum, na ni lazima kuyachuliia kama ni maisha Matakatifu yaliyowekwa wakfu kama ilivyoelezwa katika kipengere cha Mtaguso Mkuu II, Kanisa katika Ulimwengu (cf. Gaudium et Spes , 48; Familiaris Consortio , 56) . Kwa wanandoa , kwa mujibu wa Sakramenti, hii, maisha yao yanakuwa ni dhamana ya kanisa katika kutoa ujumbe wa kweli wa Injili ya upendo ,katika katika maisha ya kawaida,kama Kristu anavyolipenda Kanisa lake, linalo endelea kuwa hai , kwa ajili yake, katika uaminifu na huduma.
Papa ameuleza mpango huu wa ajabu wa asili katika sakramenti ya ndoa , wenye kufanyika kwa unyenyekevu na pia katika hali ya udhaifu wa binadamu, kwa kuwataka wanandoa kumweka Mungu kati wakati wote hata katika majaribu magumu na changamoto wanazoweza kupambana nazo. Jambo muhimu ni kuweka kiungo hai na Mungu, kuwa msingi wa dhamana ya ndoa. Familia anayosali pamoja huduma pamoja " aliandika mtumishi wa Mungu Patrick Peyton . Papa alitoa wito kwa familia kujenga tabia za kusali pamoja , tangu wanapoianza siku, kabla ya mlo, na kila inapohitajika .
Mwanzoni na mwishoni mwa siku, kabla ya milo, na katika yakati tete zaidi za maisha ... Tunaweza kusali Rozari, yenye kuleta hisia ya uwepo wa Maria, Malkia wa familia na mfano familia akiwa na mumewe Yosefu, katika familia zetu ... Na pia ni vyema kuandamana kifamilia katika maadhimisho ya Ekaristi, na hasa siku za Jumapili , kushiriki katika meza ya neno na Mwili wa Kristo, bibi na bwana harusi wa Wakristu, ambamo wanaweza kuteka nguvu ya kupendana , kusaidiana na kusameheana katika maisha ya kila siku.
Papa alikamilisha katekesi yake kwa kumshukuru Mungu kwa familia nyingi zinazodumisha uhai wa Jumuiya zetu za Kikristo, kutoa huduma muhimu na ushahidi na nguvu ya imani.
Na baada ya katekesi alisalimia makundi mbalimbali yaliyofika kumsikiliza, wakiwemo wagonjwa na maarusi wapya.








All the contents on this site are copyrighted ©.