2014-04-02 07:18:56

Ontario, Canada kumuenzi Yohane Paulo II kila mwaka


Baraza la Serikali ya Jimbo la Ontario Canada, limepitisha muswada wa sheria ambayo imeanza kutumika kwamba, kila Mwaka ifikapo tarehe 2 Aprili, wataadhimisha Siku ya Yohane Paulo II, kama kumbu kumbu endelevu ya kifo cha Papa Yohane Paulo II, kiongozi wa Kanisa aliyesimama kidete kulinda na kutetea misingi ya haki, amani, upendo na mshikamano wa kimataifa.

Hizi ni juhudi zilizofanywa na Mbunge Dipika Damerla na muswada ukapita kwa kura za kishindo na tangu tarehe 17 Machi 2014, Sheria hii imeanza kutumika na kwamba, tarehe 2 Aprili 2014 imekuwa ni siku ya kwanza tangu Sheria hii ilipopitishwa.







All the contents on this site are copyrighted ©.