Dunia yawakumbuka Watoto wenye wigo wa akili (autism)
Tarehe 2 Aprili , ni siku ya kuwakumbuka watoto wenye ulemavu au wigo wa akili . Hili
ni adhimisho la saba la Dunia kwa ajili ya watoto hao. Rais wa Baraza la Kipapa
kwa ajili ya kazi za Kichungaji kwa Wafanyakazi na wahudumu wa Afya, Askofu Mkuu Zygmunt
Zimowski, ameiadhmisha siku hii kwa na wito wa kuejnga matumaini na ushirikiano wa
dhati na familia au wale wote waliojitolea kuishi na watoto wenye ulemavu wa akili.
Na kwamba, katika maadhimisho ya Siku hili, Dunia inaonyesha huruma na na upendo
wa kina kwa watoto hao, na hivyo inakuwa ni changamoto kwa Kanisa zima kuishi ukweli
wa upendo wa Kristo kwa watu wote wakiwemo atu wenye matatizo ya wigo wa akili. Askofu
Mkuu Zimowski, amehimiza wasiokuwa namatatizo hayo katika familia zao, kuw ana moyo
wa huruma majitoleo ya sadaka ya kutoa msaada hasa wa huduma, ili wale wanaowatunza
pia wapate muda wa kufanya shughuli nyingine. Amesema familia zenye kuwa na watoto
hawa walemavu wa akili wanastahili kupata msaada wa mawazo pia na kihali, na hasa
pale panapokuwa na hisia za kukata tamaa au uwepo wa mgogoro katika mahusiano na hisia
kwamba tatizo hilo linatokana na muungano wao katika uzazi. Ni hali ngumu halisi,
inayo hitaji ushirikiano na mawasiliano na uelewa na hekima kwa familia zenye matatizo
haya.Na wapo wengi wanaokubali hali kama mpango wa Mungu. Hivyo amesisitiza Askofu
Mkuu Zimowski, ni muhimu kupambana na unyanyapaa wa aina yoyote , hasa kupitia njia
ya ushirikiano katika jamii, kuvunja vizuizi na kutengwa, na chuki zinazo tokana na
uwepo wa mgonjwa huyo, badala yake iwe ni kuimarisha uhusiano, hasa kati ya wazazi.
Na pia inaweza kufanikisha msaada wa utendaji wa jamii katika mazingira ya huduma,
habari, mawasiliano na mafunzo, kuwezesha kwa njia hii ya mpito kwa ufahamu wa kweli
na kukubalika kwa ugonjwa huo, ambayo kukanusha na kukemea hali yoyote iliyotaka kudhoofisha
hadhi ya mgonjwa.
Hivyo, inawezekana kuanzisha misingi ya matumaini kwa kutowatenga
watu wenye ugonjwa wa akili , au familia zao, ikilishwa na mizizi ya umoja, kushirikiana
na kuaminiana katika mshikamano adilifu wa kijamii. Na kwamba, mkazo mkubwa wa Kanisa,
ni kuunga mkono na kuhamasisha matumaini mapya katika uwanja wa matatizo ya wigo wa
akili .
Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya kazi za Kichungaji kwa wafanyakazi
na wahudumu wa afya, katika adhimisho la siku hii, ametangaza kwamba, mkutano wa
kimataifa wa XXIX , utakao fanyika Novemba 20-22 ijayo na Baraza, watakuwa na mkutano
huo mjini Vatican, kwa ajili ya kushughulikia mada: "Matatizo ya wigo wa akili : uwepo
wa Tumaini.