Familia ya Kikristo ni mahali ambapo watoto wanapokea tangazo la kwanza la imani.
Kwa sababu hii nyumba ya familia imeitwa kwa haki "Kanisa dogo la nyumbani", Jumuiya
ya neema na sala, shule ya fadhila za kibinadamu na mapendo ya Kikristo.
Baba
Mtakatifu Francisko kwa kutambua na kuthamini umuhimu wa Familia za Kikristo katika
maisha na utume wa Kanisa, leo katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii,
anawahimiza wazazi kuwafundisha watoto wao namna ya kusali vyema. Lakini pia anawataka
kusali pamoja na watoto wao!