Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda, Jumatatu tarehe 31 Machi 2014 amepokea maandamano
makubwa ya wananchi wa Uganda wanaounga mkono ujasiri wake wa kupitisha muswada wa
sheria unaopinga vitendo vya ushonga nchini Uganda.
Wananchi wa Uganda wanasema,
Rais Museveni ameonesha ukomavu wa kisiasa, utu na maadili mema kadiri ya mila na
mapokeo ya kiafrika na kamwe asikubali kuyumbishwa na propanda kutoka katika Nchi
za Magharibi zinazotishia kusitisha, kufuta au kukata misaada ya maendeleo kwa Uganda.
Viongozi wa dini mbali mbali nchini Uganda wamefanya Ibada ya pamoja kwa ajili ya
kumwombea Rais Yoweri Kaguta Museveni katika utumishi wake kama Rais wa Uganda.
Akizungumza
na wananchi wa Uganda, Rais Museveni anasema kwamba, Uganda haitishiki kwa nchi wahisani
kutishia kusitisha misaada yenye masharti na inayochochea vitendo vya uvunjifu wa
maadili na utu wema. Hadi sasa jumla ya dolla millioni 118 zimesitishwa kupelekwa
Uganda, tangu Rais Museveni alipotia sahihi muswada wa sheria dhidi ya vitendo vya
ushoga nchini Uganda.
Takwimu zinaonesha kwamba, Uganda ni kati ya nchi 37
kutoka Barani Afrika ambazo zinapiga rufuku ya vitendo vya ushoga. Rais Museveni anasema,
ushoga hauna tija wala mashiko kwa wananchi wa Bara la Afrika. Tukio la kumshukuru
Mungu kwa ajili ya ushupavu uliooneshwa na Rais Museveni limeandaliwa na Viongozi
wa kidini nchini Uganda.