Papa awahimiza Wasalesiani kuwaendea vijana wanyonge katika jamii
(Vatican Radio)Jumatatu 31 March 2014, majira ya asubuhi, Baba Mtakatifu Francisko,
alikutana na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 27 wa Shirika la Wasalesiani wa Don Bosco,
na kutoa shukurani zake za dhati kwa Mkuu wa Shirika, Padre Angel Fernandez Artime,
na pia kwa wanashirika wote . Alionyesha imani yake kwa uongozi wa shirika linavyo
tembea katika njia yake. Na aliwaombea Roho Mtakatifu, awawezesha kuelewa matarajio
yao na changamoto za wakati wetu, hasa kwa vijana, katika tafsiri ya mwanga wa
Injili na Karama zao, katika misingi ya majiundo ya utume wa Shirika. .
Hotuba
ya Papa, ilirejea madhari ya mkutano “kuwa Mashahidi Jasiri Injili" kama daima,
ilivyokuwa nia ya mtangulizi wao , Don Bosco, ambaye alisisitiza mawili : kazi na
kiasi. Kazi na kiasi hivyo unakuwa ni mhimili wa shirika. Papa alieleza na kuasa
dhidi ya mwelekeo wa kufikiri na kufanya kazi kwa faida binafsi, na kuanguka katika
majaribu ya kidunia. Alikumbusha utendaji wote wa shirika iwe kwa ajili ya Mambo
ya Mungu na Ufalme wake. Kisha kiasi iwe katika hisia za uwiano wa maisha ya kawaida
kwa wanashirika, wakimulikiwa na umaskini wa Don Bosco na Mama Margaret, katika kuona
umuhimu wa maisha ya msalesiani katika misingi ya maisha ya ila binadamu , na hasa
katika kuwa karibu na maskini, uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa mali .
Aidha
Papa alizungumzia Uinjilishaji wa vijana katika utume wa Roho Mtakatifu iliyekabidhiwa
kwa Kanisa, katika maana ya uhusiano wa karibu na vijana na elimu yao, wakilenga
kutembea pamoja katika safari ya kukua katika imani Kiinjili, na ukomavu wa kibinadamu.
Papa amezungumzia haja ya kuwaandaa vijana kufanya kazi katika umoja wa roho ya Injili
, kama mawakala wa haki na amani, na kuishi katika mshikamano na viongozi wao na
wakuu wa Kanisa. Na alitaja hili linahiji jambo la kwanza kabisa , sala, ndipo shughuli
za pamoja , na kisha , mipango ya kibinafsi na ujasiri wa kutoa mapendekezo na kusindikizana
katika maisha ya ushirika kama familia moja ya Wasesiani. Kujali pia mahitaji mpya
msingi kwa ajili ya majiundo, elimu uongozi na utambuzi.
Na amewahimiza Wasalesiani,
zaidi kuwaendea na kufanya kazi na vijana, wanaoonekana kusahaulika au kupuuzwa na
jamii kutokana na hali yao duni ya kimaisha. Vijana walio jitenga au kutengwa. Papa
amewaalika kuzifikiria hali halisi, hasa tatizo kubwa la ukosefu wa ajira, na matokeo
yake hasi. Na pia kufikiria juu ya utegemezi , ambayo kwa bahati mbaya,anasema mizizi
yake inatokana na ukosefu wa upendo wa kweli. Na kuwafikia vijana waliowekwa pembezoni
, kunahitaji ujasiri katika sala, maombi , ukomavu binadamu na mahusiano ya kweli.
Na kwamba kuna umuhimu wa vijana hawa kuendelea kusindikizwa mara kwa mara.
Na
Papa alimshukuru Mungu kwa uwepo wao na kwa kufanya kazi zao, ambazo huzifanya si
kama mtu binafsi, lakini kama jumuiya, wakidumisha kila utendaji wa kitume katika
karama za mwanzishi wao . Na ameasa dhidi ya hatari za mivutano ya ndani am bayo hasa
misingi yake ni ubinafsi , akiomba waione haja ya kuwa mawasiliano ya kina na mahusiano
halisi miongoni mwao. Na kwa nguvu ya kuimwilisha Injili, wataweza kuishi kwa udugu
aliishi, kuheshimiana, kusaidiana , kuelewana , kutendeana kwa wema, msamaha na furaha
. Roho wa familia Don Bosco wanayorithi , ni msaada mkubwa katika maana ya kuwa na
moyo uvumilivu na ujenzi wa ubunifu katika maisha yaliyowekwa wakfu. Na aliwatakia
kila la heri kwa ajili ya maadhimisho ya kutimia miaka mia mbili ya kuzaliwa kwa
Don Bosco.Pia aliwaombea msaada wa Mama Maria , Msaada wa Wakristo, ambaye hajawahi
kushindwa kutoa misaada yake, kwa wanaomkimbilia.Kwa Maombezi yake ya kimama, Mungu
hutoa matunda yanayotarajiwa. Na aliwapa Baraka zake za Kipapa, na kuwaomba wamwobee
pia.