Kwaresima ni kipindi cha kubadili mwelekeo wa maisha!
Kwaresima ni kipindi na mwaliko wa toba, wongofu wa ndani, sala na tafakari ya kina
ya Neno la Mungu, linalomwilishwa katika huduma ya mapendo kwa jirani. Ni kipindi
cha kukimbilia huruma na upendo wa Mungu kwa njia ya Sakramenti ya Upatanisho, inayomwonjesha
mwamini ile furaha, huruma na upendo wa Baba ambaye daima anasubiri kuwaona watoto
wake waliokimbia kutoka nyumbani, wakirejea kwa toba na unyenyekevu wa moyo!
Baba
Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii anasema,
kwamba, Kwaresima ni kipindi cha kubadilisha mwelekeo wa maisha, kwa kupambana kufa
na kupona na ubaya pamoja na umaskini wa maisha ya kiroho, kihali na kipato.