2014-03-29 15:45:56

Uteuzi katika Mabaraza ya Kipapa!


Baba Mtakatifu Francisko ameridhia uteuzi wa Kardinali Joao Brazi de Aviz kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mashirika ya Kitawa na Kazi za Kitume pamoja na kuteuwa baadhi ya wajumbe wapya kwenye Baraza hili. Papa pia ameridhia uteuzi wa Kardinali Jean Louis Tauran na Padre Miguel Angel Ayuso Guixot kuwa ni Rais na Katibu mkuu wa Baraza la Kipapa na Majadiliano ya Kidini pamoja na kuwateua baadhi ya wajumbe wapya ili kuongeza nguvu katika majadiliano ya kidini.

Wakati huo huo, Baba Mtakatifu Francisko ameridhia uteuzi wa Kardinali Gianfranco Ravasi, Askofu mkuu Carlos Alberto de Pinho Moreira Azevedo pamoja na Askofu mkuu Barthèlemy Adoukonou kuwa ni Rais, Mwakilishi na Katibu mkuu wa Baraza la Kipapa la Utamaduni.







All the contents on this site are copyrighted ©.