2014-03-28 10:54:44

Kwaresima iwasaidie kupambana na mapungufu yenu ya kibinadamu!


Kwaresima ni kipindi cha toba na wongofu wa ndani; ni muda muafaka wa kufanya tafakari ya kina ya Neno la Mungu, inayomwilishwa katika matendo ya huruma. Ni kipindi cha mapambano katika maisha ya kiroho, ili kujiandaa na kuwa tayari kuadhimisha Fumbo la Pasaka, yaani mateso, kifo na ufufuko wa Kristo.

Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii anasema kwamba, kila mwamini anapaswa kuboresha maisha yake kwa kuwa mtu mwema zaidi. Kipindi cha Kwaresima kiwasaidie waamini kupambana na mapungufu yao ya kibinadamu!







All the contents on this site are copyrighted ©.