2014-03-27 14:34:49

Viwawa yahimiza vijana kuungana katika mapambano dhidi ya ukosefu wa ajira.


Vijana Wakristu wafanya kazi duniani kote wanahimizwa kujiunga katika vikundi mbalimbali vya utendaji kwa ajili ya kupambana na ukosefu wa ajira, umaskini na utegemezi. Himizo hilo limetolewa Alhamis hii na Monica Wanjiru, wa Kitengo cha Afrika katika Shirika Katoliki la Kimataifa, kwa ajili ya kuratibu shughuli mbalimbali za vijana Wakatoliki duniani(VIWAWA) , lenye Makao yake Makuu hapa Roma. .

Monica Wanjiru ameeleza juu ya juhudi hizi za Vijana Wakristu wafanya kazi(VIWAWA)kwamba ni mfumo unao unganisha pamoja vijana, licha ya tofauti za hali, kazi na mazingira. Lengo Kuu la VIWAWA, ikiwa ni kusaidia kuwaleta pamoja vijana, kutafakari na kuchukua hatua wenyewe ,na kwa uhuru wao kamili, kukabiliana na yale yanayokuwa changamoto zinazo wazuia kuishi maisha ya heshima na katika kutoa ushuhuda wao kwa uwepo wa Mungu katika Mpango wake kupitia Yesu Kristo katika dunia ya kazi kwa vijana.

VIWAWA husaidiwa na Mapadre na Masista na walei pia ,ambao huwasindikiza na kuwasaidia katika utume wao. Na kwamba , utendaji huu wa pamoja licha ya kuwafanikisha vijana kuishi maisha ya kuheshimika ,pia husaidia kuona na kutoa msaada unahotajika kwa vijana wengine, kiroho na kihali ,na hivyo kufanikisha mabadiliko ya kimaisha, yaliyojengwa katika misingi ya upendo na amani ya Mungu Mwenyezi kati yao.

Monica Wanijru, raia wa Kenya, ni kati ya Waratibu wa shughuli za Vijana , katika Makao Makuu ya VIWAWA, yaliyopo hapa Roma. Katika mahojiano na mahojiano na Redio Vatican, alielezea juu ya juhudi hizi, akianza na kujitambulisha mwenyewe .. RealAudioMP3







All the contents on this site are copyrighted ©.