2014-03-27 11:04:24

Msaada kwa wananchi wa Ufilippini!


Askofu mkuu Joseph Kalathiparambil, Katibu mkuu wa Baraza la Kipapa la wahamiaji na watu wasiokuwa na makazi maalum, kuanzia tarehe 15 hadi 29 Machi 2014 pamoja na ujumbe wake, wamekuwa nchini Ufilippini, kuzindua mradi wa upendo na mshikamano kwa wananchi walioathirika kwa tufani ya Hayan, iliyotokea nchini humo, Mwezi Novemba 2013 na kusababisha maafa makubwa kwa watu na mali zao.

Miradi ya mshikamano wa upendo na kidugu, inafadhiliwa na mchango kutoka kwa waamini na watu wenye mapenzi mema iliyokusanywa na Baraza hili kwa ajili ya kuwasaidia wavuvi na familia zao kurudia tena maisha ya kawaida. Akiwa nchini Ufilippini, Askofu mkuu Kalathiparambil amekutana na kuzungumza na viongozi wakuu wa Kanisa, Shirika la Misaada la Kanisa Katoliki, Caritas na wahusika wenyewe, ili kuangalia jinsi ya kutekeleza miradi hii kwa ufanisi mkubwa zaidi.







All the contents on this site are copyrighted ©.