2014-03-26 14:47:37

Askofu Tebartz-Van Elst kupangiwa kazi nyingine!


Baada ya viongozi wa Kanisa kufanya uchunguzi wa kina kuhusu tuhuma za ubadhirifu wa mali ya Kanisa uliofanyika Jimbo Katoliki la Limburg, Ujerumani, imeamriwa kwamba, Askofu Franz-Peter Tebartz-Van Elst, hana tena sifa za kuweza kuongoza Familia ya Mungu Jimboni humo.

Vatican imekubali ombi la kung'atuka kutoka madarakani lililowasilishwa na Askofu Franz-Peter na hivyo, Askofu Manfred Grothe ameteuliwa kuwa Msimamizi wa Kitume. Baba Mtakatifu anaiomba Familia ya Mungu Jimboni humo kuupokea uamuzi huu kwa moyo mkunjufu na kwamba, Askofu Tebartz-Van Elst, atapangiwa kazi nyingine.







All the contents on this site are copyrighted ©.