2014-03-22 10:31:48

Yesu ni tumaini letu!


Matumaini ni fadhila ya Kimungu inayomwezesha mwamini kutamani heri ya Ufalme wa mbinguni na uzima wa milele, kwa kutumainia ahadi za Kristo na kutegemea, siyo nguvu zao, bali msaada wa neema ya Roho Mtakatifu. "Na tulishike sana ungamo la tumaini letu, lisigeuke; maana Yeye aliyeahidi ni mwaminifu".

Fadhila ya matumaini inajibu tamaa ya heri iliyowekwa na Mungu katika moyo wa kila mtu. Yachota matumaini yanayovuvia matendo ya watu. Huyatakasa ili kuyapanga kwa ajili ya Ufalme wa mbinguni nyakati za upweke. Hufungua moyo katika kungoja heri ya milele. Akielekezwa na matumaini anakingwa na ubinafsi na anaongozwa kwenye furaha itokanayo na upendo.

Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii anawakumbusha kwamba, Yesu ndiye tumaini lao. Hakuna kitu chochote iwe mateso au kifo kinachoweza kuwatenganisha nguvu ya upendo wa Mungu unaookoa.







All the contents on this site are copyrighted ©.