2014-03-22 15:40:59

Papa akutana na familia za wahanga wa mafia.


(Vatican Radio) Ijumaa jioni Papa Francisko alikutana na familia za kafara waliouawa katika utendaji wa mtandao wa chama cha kisiri cha mafia. Na aliwahimiza wanachama wa mafia, kubadili mienendo ya maisha yao, waongoke na kutafuta huruma ya Bwana kwa dhambi zao. Papa alitoa ombi hilo, akiwa katika Parokia ya Mtakatifu Gregory VII, ambako aliongoza Mkesha wa sala za jioni, kama ilivyokuwa imeandaliwa na chama cha Libera Foundation.

Papa Francisko kabla ya kuwahutubia, alisikiliza kwa hali ya ukimya orodha ya majina 842, wahanga wa vurugu za mafia, wakiwemo watoto 80, majina yaliyozomwa moja baada ya jingine. Papa alionyesha kuelewa uchungu wa watu 700 walioshiriki rasmi katika tukio hii , wengi wao wakiwa ni kutoka familia zilizopoteza wapendwa wao, na hivyo aliombea huruma ya Mungu na mshikamano wa dhati katika kuona madhara ya chama hiki batili cha mafia.

Papa aliwapongeza wote walioshiriki na kutoa ushuhuda wao, na ujasiri wa kushiriki mateso yao na mateso ya wengine na kwa matumaini yao kwamba, Ipo siku uovu huy wa rushwa utashindwa.

Na kisha Papa Francisko, alikemea na kuwaonya wanaume na wanawake wanao shiriki au kuendeleza mtandao huu mbovu wa mafia, akiwataka wabadilike kimaisha.Wafuate njia ya upendo na huruma inayoonyeshwa na Bwana, na kusitisha maovu katika jamii.

Papa kwa uchungu aliwaombea huruma ya Mungu hasa wale waliuawa bila hatia.Na kwa wale wanaoendeleza ukatili huu alisema, napiga magoti chini, nakumuomba kila msharika wa mafia, abadilike na kuwa mtu mwema , maana wema wao kimaisha , ni furaha ya jamii nzima. Na wakumbuke kwamba, mamlaka na fedha, walizo jipatia kwa njia ya shughuli nyingi chafu ,na uhalifu mwingi wa mafia - ni fedha za damu na ni mamlaka ya damu ambayo ufahali wake ni wa muda mfupi na hauwezi kuwafikisha katika furaha ya milele.

Papa aliendelea kuwataka waongoke , na kwamba wanayo nafasi ya kufanya hivyo, ili wasiishie katika moto wa Jehanamu. Na kwamba hakuna cha maana cha kusubiri katika njia hiyo mbovu, bali wakate shauri mara na kuondokana na njia hiyo na kujiunga katika njia nyingine ya amani na utulivu. Aliwaaka wawafikirie wazazi wao, ndugu zao , marafiki na jamii iliyoteseka kutokana na utendaji wa mafia. Wajutie dhambi zao na kuongoka . Wabadilishe mwenendo wao wa maisha.

Papa alihitimisha hotuba yake, kwa kuongoza sala ya Salaam Maria, ikifuatiwa na Sala ya Baba Yetu.

Mkesha wa huu wa sala na maombi, ulifanyika siku moja kabla ya kutimia kumbukumbu ya 19 kwa ajili ya uwajibikaji na kumkumbuka kwa waathirika wasio na hatia katika uhalifu wa kupangwa. Aidha Jumamosi, mamia watu wameandamana katika mji wa Latina, Kusini mwa Roma, na kisha kushiriki katika warsha juu ya "vipi jamii inaweza kuwa na utendaji ulio bora zaidi kwa ajili ya kusitisha matendo mabovu ya mafia", amba yo hasa ni rushwa.








All the contents on this site are copyrighted ©.