2014-03-22 11:55:47

Caritas inaendelea kuwasaidia waathirika wa vita nchini Mali


Shirika la Misaada la Kanisa Katoliki Italia, Caritas Italia, linaendelea kutoa msaada wa hali na mali kwa waathirika wa vita iliyotokea nchini Mali kunako Mwaka 2012 hadi Mwaka 2013. Hadi sasa bado kuna idadi kubwa ya wakimbizi na watu wasiokuwa na makazi wanaoendelea kupata msaada kutoka katika Mashirika ya misaada ya Kimataifa.

Hivi karibuni, viongozi wa Kanisa nchini Mali waliomba msaada wa dharura kwa ajili ya kusaidia kuwahudumia wakimbizi na watu wasiokuwa na makazi wanaoendelea kuishi kambini. Mashirika mbali mbali ya misaada ya Kanisa Katoliki yamekwisha kuchangia msaada kwa watu 65, 000. Caritas inatoa msaada pia Niger na Burkina Faso.







All the contents on this site are copyrighted ©.