2014-03-21 13:13:25

Vyama vya wakulima duniani kukutana nchini Argentina


Shirikisho la Wakulima Duniani, WFO, litakuwa na mkutano wake mkuu wa Mwaka kuanzia tarehe 25 hadi tarehe 29 Machi 2014 huko Buenos Aires Argentina. Chama cha Wakulima Vijijini nchini Argentina ndio wenyeji wa mkutano huu unaotarajiwa kuhudhuriwa na vyama 100 vya wakulima kutoka katika nchi 80 duniani.

Wajumbe wa mkutano huu wataweza kushirikishana changamoto zinazojitokeza katika sekta ya kilimo duniani, ufugaji endelevu, maboresho ya mikataba ya kilimo, mabadiliko pamoja na athari za mabadiliko ya tabianchi. Mkutano wa Shirikisho la Wakulima Duniani utafunguliwa rasmi hapo tarehe 26 Machi 2014.

Itakumbukwa kwamba, mkutano huu unafanyika wakati ambapo Jumuiya ya Kimataifa inakazia umuhimu wa kuwekeza katika sekta ya kilimo ili kuinua hali ya maisha ya familia nyingi vijijini sanjari na kuhakikisha kwamba kuna usalama wa chakula duniani. Jumuiya ya Kimataifa inaendelea kuhamasishwa kutunga sera bora za kilimo zinazowashirikisha wanawake kwa kuwajengea uwezo katika elimu, masoko na haki msingi.








All the contents on this site are copyrighted ©.